TEZI DUME NA SARATANI YA TEZI DUME
Tezi dume ni nini?
Tezi dume ni tezi inayopatikana kwa jinsia ya kiume.
Tezi hii ina kazi ya kutengezeza majimaji meupe mepesi yenye unato kidogo.
Majimaji haya husaidia mbegu za kiume kutembea kwa urahisi.
Iko wapi
Tezi dume iko mwishoni mwa kibofu cha mkojo.
Pia inauzunguka mrija unaounganisha kibofu cha mkojo na mrija wa mkojo wa uume (urethra) na iko mbele kidogo ya utumbo mpana ndani ya fupa la nyonga.
Saratani ya tezi dume ni nini?
Saratani ya tezi dume maana yake ni tezi dume imepata ugonjwa wa saratani..Na hii hutokea pale ambapo, chembechembe hai za tezi na kuanza kujigawanya bila kufuata utaratibu wa mfumo wa mwili, chembechembe hai hizi mwishowe hutengeneza vivimbe hatari ndani ya tezi dume na hatimaye husambaa mwilini
Visababishi hatarishi kwa saratani ya Tezi dume
Umri Mkubwa kuanzia miaka 50
Nasaba (ukoo wenye historia a saratani hii
Lishe hatarishi-nyama nyekundu kwa wingi, mafuta/samli, na Vyenginevyo.
Unene uliokithiri/Uzito uliyozidi / wa kuwa na kitambi.
Ukosefu wa mazoezi
Upungufu wa virutubisho,mfano vit D,na Vyenginevyo.
Kutokupata choo kikubwa inavyotakiwa.
Maambukizi ya mara kwa mara kwenye tezi dume
Dalili zake ni zipi?
Kuna dalili nyingi ila hizi Ni baadhi tu*
1 Udhaifu katika utoaji wa mkojo, mkojo hauishi.
2 Kwenda kukojoa mara kwa mara.
3 Damu ndani ya mkojo.
Kushindwa kukojoa.
4 Maumivu ya kiuno na mifupa ya nyonga.
5 Wagonjwa wengi huanza maumivu ya nyonga kama ni dalili za awali.
6 Udhaifu katika utoaji wa mkojo pia kunaweza kutokea kwa kuvimba kwa tezi dume bila ya saratani.
7 Damu kwenye mkojo nakushindwa kumaliza mkojo ni ishara tosha ya kuwa tezi dume imeathirika.
UCHUNGUZI
Wanaume wote wanapaswa kufanya uchunguzi wa saratani ya tezi dume kuanzia miaka 20.kwa wakati huu tulonao,kwa Wakati wa zamani ilikuwa tatizo hili huanza mtu kulipata akiwa na Umri wa miaka 50,na ndio huwaza kufanya vipimo na ushauri nasaha wa kutibu tatizo.
Kwa wale wenye historia katika familia wanapaswa kuanza wakiwa na umri wa miaka 45.
MADHARA YA MATIBABU YA TEZI DUME KWA UPASUAJI AU MIONZI
👉Kuzuia mkojo
👉Kupoteza nguvu za kiume.
👉Homoni huongeza joto mwilini.
👉Kupungukiwa na nguvu za kiume.
👉Kupata kidonda kwenye Tezi dume,hupelekea kuwa ndio tatizo la kudumu.
👉Kutokuwa na hisia za mapenzi Yaani kuwa hudisi Uume hausimami,(Hanithi).
👉Utapaki kuvaa pempasi au mipira ili kuzuia mikojo kutoka Ovyo na Mengineo.
Kwa ushauri/matibabu Zaidi Wa Kiafya Wasiliana Nasi;
.............0714100697
