TEZI YA BATHOLIN NI NINI
Hizi ni tezi zisizoonekana zipo kkwenye mashavu ya uke sehemu ya chini karibu na tundu la uke.
Tezi hizi husaidia kuzalisha ute ili kuufanya uke kuwa na unyevunyevu muda wote.
Uvimbe katika viungo vya nje vya uke hutokea tu au husababishwa na maambukizi. Uvimbe huu unaweza kuwa na maumivu au usiwe na maumivu. Uvimbe unaweza kuwa mdogo au mkubwa kutegemea na sehemu ulipo na muda tangu ulipoanza.
Mwanamke pia anaweza kupata tatizo la midomo ya ndani ya uke ambayo hurefuka na kujiona kama kero, hiyo ni hali ya kimaumbile na haina madhara.
AINA ZA UVIMBE
Uvimbe wa mashavu ya uke huwa unatokea kwenye tezi iitwayo ‘Bartholin gland’. Tezi hii huwa haionekani kwa macho na mojawapo ya kazi zake ni kutoa majimaji ya kulainisha uke wakati wa tendo la kujamiiana.
⏩Bartholin cyst‘, huu ni uvimbe mgumu hutokea pembeni ya shavu la uke kwa ndani. Uvimbe huu mara nyingi huwa hauumi lakini huendelea kukua na kuleta shida wakati wa tendo la kujamiiana, na hutokea tu wenyewe. Uvimbe huonekana kwa macho au mwanamke anauhisi anaponawa ukeni au wakati wa kujamiiana. Uchunguzi wa kina hufanyika ili kuangalia uhusiano wake na sehemu nyingine za mwili. Matibabu ya aina hii ya uvimbe ni upasuaji wa kuondoa kabisa.
⏩ *Bartholin Abscess* Aina hii ya uvimbe ni jipu kwani ndani yake huwa kuna usaha. Uvimbe huu huwa na maumivu makali sana, hutokea upande mmoja wa shavu la uke. Mgonjwa pamoja na kuwa na maumivu makali huweza kupata homa, kushindwa kutembea vizuri na wakati mwingine uvimbe hupasuka. Maumivu husababisha mgonjwa ashindwe kuendelea na mambo yake.
Matibabu ya uvimbe huu ni upasuaji na kuondoa usaha wote kisha kurekebisha kingo za kidonda kitaalamu, hili lisipofanyika, jipu hili huwa na tabia ya kujirudia rudia.
Athari ya aina hii ya uvimbe ambayo ni jipu ni maumivu makali, kushindwa kufanya tendo la ndoa na uvimbe unapasuka na kusababisha kidonda.
*Kuna sababu kubwa zinazofanya mtu atokwe na uvimbe huu*
1. Maambukizi ya Bacreria anayeutwa E- coli ambapo anakuja na kuziba njia za kwenye maingilio ya glands hzo
2. Maambukizi ya magonjwa ya zinaa kama kisonono na chlamydia
Ukiona dalili zifuatazo ni ishara ya kuwa una tatizo la Bartholin Abcess/ cyst.... yaani uvimbe kwenye mashavu ya uke karibu na mlango wa uke.
1. Umeota Kiuvimbe kwenye mashavu karibu na mlango wa uke
.
2. Unapata maumivu makali sana wakati mwingine unapata shida hata kutembea au kukaa
.
3. Inakuwa ngumu kufanya tendo la ndoa kwa sababu ya maumivu
.
4. Uke wako unakuwa mkavu.
.
5. Wakati mwingine inaweza kukusababishia homa
Tatizo linatibika
𝐓𝐮𝐰𝐚𝐬𝐢𝐥𝐢𝐚𝐧𝐞 𝐥𝐞𝐨 𝐧𝐨.0714100697
